Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Magufuli: CCM imefanya kampeni za kistaarabu

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BUREBy Herieth Makwetta, Mwananchi hmakweta@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mgombea wa urais wa CCM, John Magufuli amesema viongozi, wagombea na wafuasi wa chama hicho walifanya kampeni za kistaarabu, huku akilisifu Jeshi la Polisi kulinda amani.


Magufuli amesema hayo leo Jumanne Oktoba 27, 2020 wakati akizungumza na wazee wa mkoa wa Dodoma na waandishi wa habari katika ukumbi wa Convetion Center jijini Dodoma.


Amesema miezi miwili ya kampeni wametembea na kukutana na wananchi nchi nzima.


“Tumefanya kampeni za ustaarabu sana, upendo na kumtanguliza Mungu mbele katika maslahi mapana ya nchi yetu, asanteni sana. CCM imesimamisha wagombea wengi nchi nzima ukilinganisha na vyama vingine, viongozi na wagombea wa CCM, wasanii, wanamuziki, waigizaji, wameipigia kampeni CCM kupitia mitandao yao ya kijamii, ninawashkuru sana,” amesema Magufuli.


Ameongeza, “Tulijikita kuelezea mambo yaliyopo kwenye ilani, tumewaleza wananchi mambo tuliyoyafanya na  tunayotarajia kuyafanya miaka mitano ijayo.”


Amesema jeshi la polisi limefanya kazi kwa weledi mkubwa bila kutetereka, licha ya kuchokozwa na baadhi ya watu waliotaka kuvunja amani.


“Najua kuna nyakati walichokozwa, lakini hawakukubali kuchokozeka. Hongera kwa jeshi la polisi kwa kazi ya ulinzi na usalama, wamefanya kazi kubwa katika kipindi hiki chote cha kampeni,” amesema.


Pia amesema kitendo cha wananchi kujitokeza kwa wingi katika mikutano yao ya  hadhara imeonyesha kuwa Tanzania ipo juu na ipo imara.

Post a Comment

0 Comments