Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Familia Yamuondoa Gadiel Simba SC

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroek, amesema beki wa timu hiyo, Gadiel Michael amepata matatizo ya kifamilia jambo ambalo linamfanya akosekane ndani ya kikosi.

 

Gadiel amekuwa akikaa benchi kwa muda mrefu baada ya nafasi yake kuchezwa na Mohammed Hussein ambaye ni chaguo namba moja la Sven.

 

 

Kocha huyo aliyazungumza hayo baada ya kumalizika kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya African Sports ya Tanga inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza uliopigwa Jumatatu.

 

“Tumempa ruhusa Gadiel kutokana na matatizo ya kifamilia aliyonayo lakini atajiunga na timu hivi karibuni,” alisema Sven. Mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salaam, ilishuhudiwa ikimalizika kwa suluhu.

Leen Essau, Dar es Salaam

Post a Comment

0 Comments