Haijawahi Kutokea..Ndege ya Airbus Yatua Dodoma Kwa Mara ya Kwanza

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


By Sharon Sauwa, Mwananchi ssauwa@mwananchi.co.tz

Dodoma. Ndege kubwa ya Airbus A220-300 yenye uwezo wa kuchukua abiria 132, imetua kwa mara ya kwanza katika uwanja wa ndege wa Dodoma baada ya njia za kurukia kuongezwa hadi urefu wa kilometa 2.8.


Ndege hiyo iliyopewa jina la ‘Ngorongoro Hapa Kazi’ inayomilikiwa na Serikali, imekodishwa kwa Shirika la Ndege nchini (ATCL), ilitua jana saa 10:43 jioni na kupokewa na katibu mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk Leonard Chamuriho.


Baada ya ndege hiyo kutua ilipokelewa kwa kurushiwa maji na magari ya Zimamoto yaliyokuwa uwanjani hapo.


Akizungumza jana, mtendaji mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroads), Patrick Mfugale alisema Serikali iliamua barabara hiyo ya kurukia ndege irefushwe kufikia urefu wa kilometa 2.8 ili ndege za aina hiyo ziweze kutua.


“Hiyo ilifanyika makusudi ili kuwe na ufanisi katika ‘ku oparate’ ndege zetu. Kazi hii tulianza Julai mwaka huu kwa gharama ya Sh3.506 bilioni,”alisema.


Pia alisema kazi hiyo ilihusisha ujenzi wa eneo la maegesho ya ndege hiyo ambayo ina mabawa.


Pia Soma

Magufuli: Hiki ni kipindi changu cha mwisho

Magufuli: Hiki ni kipindi changu cha mwisho

Algeria wapiga kura ya maoni kubadilisha katiba

Algeria wapiga kura ya maoni kubadilisha katiba

 Kampeni za urais Marekani zapamba moto dakika za mwisho

Kampeni za urais Marekani zapamba moto dakika za mwisho

 Watu 27 wapoteza maisha Uturuki kwa tetemeko la ardhi

Watu 27 wapoteza maisha Uturuki kwa tetemeko la ardhi

ADVERTISEMENT

Alisema walilipa fidia ya Sh 5.8 bilioni kwa watu ili kupisha ujenzi huo na kwamba sasa kazi iliyobaki ni kuweka taa ili kuiwezesha ndege hiyo kutua hadi usiku.


Naye Dk Chamuriho alisema kabla ya kukarabatiwa kwa uwanja huo, ulikuwa na uwezo wa kutua ndege aina ya Bombardier yenye uwezo wa kubeba abiria 76.


Hata hivyo, alisema baada ya ukarabati imewezesha ndege hiyo kubwa inayobeba abiria 132 kutua katika uwanja huo.


“Uwanja ulijengwa kwa awamu mbili, lakini pia walilipa fidia kwa watu kupisha maeneo yao kwa awamu tatu ambapo Sh11.6bilioni zilitolewa.


Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge alisema kabla ya maboresho ya uwanja huo mwaka 2017, kulikuwa na ndege ndogo zilizokuwa na uwezo wa kubeba abiria 12.


Alisema nauli ilikuwa Sh530,000 kwenda tu, lakini sasa gharama zimepungua hadi Sh260,000 kwa mtu mmoja.


Mambo muhimu kuhusu Airbus A220-300


Ndege hiyo urefu wake ni mita 38.7, na kwa jumla inaweza kuketi abiria 141.


Urefu wake kutoka chini kwenda juu ni mita 11.5, na upana wa mabawa ni mita 35.1.


Airbus 220-300 inaweza kusafiri umbali wa 5,920km safari moja, na inaweza kupaa ikiwa na uzani wa tani 67.6, na kutua ikiwa na uzani wa tani 58.7.


Ndege hiyo ni miongoni mwa ndege za familia ya A220 na iliundwa kulenga soko la safari za ndege zinazowabeba abiria kati ya 130-160.


Ni ndege iliyounda kupunguza gharama ya matumizi ya mafuta kwa kila safari.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad