Kimenuka..Wagombea Walioshindwa na Kukimbilia Kurundikana Dar Watakiwa Kurudi Majimboni Mwao, LA sivyo....KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa, amewataka wagombea ubunge kutoka mikoani walioshindwa katika uchaguzi, warudi majimboni kwao kwa sababu kitendo cha kukusanyika jijini humo ni uchokozi wa dhahiri kwa wakazi wa jiji hilo.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Novemba, 2, 2020, wakati akizungumza kwenye kipindi cha Kumekucha cha kituo cha televisheni cha ITV, na kuongeza kuwa kitendo cha wao kuendelea kukaa jijini Dar es Salaam, ni makosa kwa sababu hawajashindiwa jijini humo.


“Walioshindwa warudi majimboni mwao kwa sababu hawajashindiwa hapa, tungependa tubaki na waliokuwa wanagombea nafasi zao na wafuate taratibu, oparesheni bado inaendelea na wote hawa ambao wametoka mikoani na wako Dar es Salaam hapa ikiwemo akina Sugu tunaendelea kuwafuatilia na ndani ya muda mfupi tutawatia mbaroni,” amesema SACP Mambosasa.


Aidha  ameongeza kuwa, “Uharamu wa maandamano haya hawakutoa taarifa kwa jeshi la polisi, badala yake wanahamasishana chini kwa chini kufanya maandamano na kufunga barabara za jiji ili wananchi washindwe kufanya shughuli zao, hakuna atakayeruhusiwa kufanya mikusanyiko wala maandamano yasiyo halali.”


 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE