11/22/2020

Kiungo Mpya Simba Atengewa Mil 300
TAARIFA kutoka ndani ya Klabu ya Simba zinasema kuwa, uongozi wa klabu hiyo umetenga zaidi ya Sh milioni 300 kwa ajili ya kumsajili kiungo mpya, Anthony Akumu raia wa Kenya.

 

 

Simba inataka kujiimarisha zaidi katika eneo la kiungo baada ya Gerson Fraga kuumia na taarifa zikitoka kwamba anaachwa na klabu hiyo. Mwishoni mwa wiki iliyopita, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Mohamed Dewji ʻMoʼ, aliweka bayana mpango wao wa kumsajili kiungo atakayekuja kuziba pengo la Fraga, ambapo akaahidi muda wowote kuanzia sasa watamtangza.

 

 

Spoti Xtra limepenyezewa taarifa sahihi kutoka ndani ya Simba, kuwa hatimaye miamba kutoka Mji wa Soweto kule Afrika Kusini, Kaizer Chiefs inayommiliki mchezaji huyo, wamemruhusu kiungo huyo atue msimbazi kwa dau nono la zaidi ya shilingi milioni 300.

 

 

“Habari ambayo ninaweza kukupatia kwa sasa ni juu ya uwepo wa ukamilishaji wa usajili wetu katika upande wa kiungo, ambapo bila shaka tumefi kia hatua ambayo tunaweza kusema kuwa tumemalizana na kiungo mkenya anayekipiga Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.

 

 

“Tunashukuru sasa tunaenda kuongeza mchezaji mwenye uwezo na mwenye umri sahihi katika safu hiyo ya kiungo mkabaji, kwani ameonyesha mambo makubwa tangu alipokuwa Zesco kabla ya kuhamia Kaizer Chiefs.

 

 

Kiasi cha zaidi ya Sh milioni 300 kimewekwa kama dau lake la usajili,” kilisema chanzo hicho. Hivi karibuni, chanzo kingine kutoka ndani ya Simba, kililiambia Spoti Xtra kuwa: “Kocha tayari alishaleta mapendekezo ya usajili wa mchezaji kwenye eneo la kiungo mkabaji na jina la Akumu lipo kati ya wale ambao amewahitaji.

 

 

Nadhani kwa kuwa aliwahi kumuona wakati akiwa Zambia, yaani Sven akiwa kocha wa Timu ya Taifa ya Zambia na Akumu akiichezea Zesco. “Bado pia kuna majina mengine mawili ya wachezaji maana jumla yapo majina matatu ambayo mwalimu ameyapendekeza, hivyo ni jukumu la viongozi kuhakikisha tunampata mmoja wapo ambapo mwalimu anaamini yeyote ambaye tutampata basi atakuwa sahihi kwake.”


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger