Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Liverpool Kama 'Sikio la Kufa Lisilosikia Dawa'

 


Beki wa kati wa liverpool Joe Gomez, ameripotiwa kupata majeraha makubwa katika mwili wake, hivyo anatazamiwa kukaa nje kwa muda mrefu.

 

Gomez ameumia akiwa katika majukumu ya timu ya Taifa ya England, inayojiwinda na michezo kadhaa wiki hii, ukiwemo ule wa kirafiki dhidi ya North Ireland alhamis hii ya tarehe 12 Novemba,


Kocha mkuu wa timu ya England Gareth Southgate, amesema ''majeraha yake ni makubwa lakini bado sifahamu itamchukua muda gani kukaa nje ya uwanja, jambo hili limenihuzunisha sana, kwa kuwa alikuwemo sehemu ya mipango yangu''.


Kwa upande wa Liverpool na Jurgen Klopp kwao si taarifa nzuri hata kidogo, kwa kuwa safu yake ya ulinzi imekumbwa na majeruhi wengi, yanaowalazimu baadhi ya nyota wake kutoonekana kwa muda mrefu, akiwemo Virgil van Dijk na kiungo Mbrazil ambaye amekuwa akichezeshwa katika safu ya ulinzi kama mbadala wa Van Dijk.


Kukosekana kwa wachezaji hawa watatu muhimu katika kikosi cha Liverpool, Van Dijk, Fabinho na Joe Gomez kunauweka ubingwa wake rehani walioutwaa msimu wa 2019-2020.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments