Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Malawi yamuachia Huru Nabii Milionea Aliyekiuka Masharti ya Dhamana Afrika Kusini

 

Nabii milionea wa Malawi Shepherd Bushiri na mke
wake wameachiwa bila masharti yoyote na mahakama moja mjini Lilongwe nchini Malawi baada ya kujisalimisha kwa polisi Jumatano.

Afrika Kusini inataka ikabidhiwe wawili hao kwa kukiuka masharti ya dhamani nchini humo.


Bushiri na mke wake wameshtakiwa nchini Afrika Kusini walikokuwa wanaishi kwa makosa ya utakatishaji wa fedha na ulaghai.


Hata hivyo wawili hao wamekanusha mashtaka hayo.


Wakili wao, Wapona Kita, aliitaka mahakama iwaachilie wawili hao bila masharti yoyote akisema kuwa kukamatwa kwao ni kinyume na sheria.


Mwendesha mashtaka aliomba mahakama kuruhusu polisi kuendelea kuwashikilia wanandoa hao kwa siku 30 zaidi ili kuwezesha Afrika Kusini kuwasilisha rasmi ombi lao la kutaka wakabidhiwe kwa nchi hiyo.


Bwana Kita alisema ni kinyume cha sheria kumzuilia mtu wakati Afrika Kusini haijawasilisha ombi rasmi.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments