Mavituzi’ ya Carlinhos Yamuacha Hoi Kaze
KOCHA Mkuu wa Yanga, Mrundi, Cedric Kaze, ametaja sifa alizonazo kiungo wake mshambuliaji, Carlos Fernandez ‘Carlinhos’.

 

Carlinhos raia wa Angola kwenye mchezo wa kwanza kuanza chini ya Kaze aliweza kufunga bao moja na aliyeyusha dakika zote 90 ndani ya uwanja.

 

Staa huyo mpya ndani ya Yanga, amefanikiwa kufunga mabao mawili, huku akipiga asisti mbili, zote zilitokana na mipira ya kona ndani ya Ligi Kuu Bara msimu huu.

 

Kaze amesema kuwa mchezaji wake Carlinhos ni mahiri katika kupiga pasi fupi na ndefu zinazofika kwa usahihi kwa wenzake.

 

Pia uwepo wa ndani ya 18 muda wote wakati timu ikishambulia ni sifa ya kiungo huyo ambaye amekuwa kipenzi cha mashabiki wa Yanga kwa muda mfupia ambao amekuwa ndani ya kikosi hicho.

 

Aliitaja sifa nyingine ya tatu ni uwezo wake wa kupiga mipira ya faulo na kona ambayo mingi anayoipiga mazoezini na kwenye mechi imeonekana kuzaa matunda.

 

“Mara nyingi nimekuwa nikimzungumzia Carlinhos, ukweli ni mchezaji wa kipekee mwenye faida kwenye timu ambaye uwepo wake uwanjani unaipa matokeo mazuri timu.

 

“Carlinhos anaweza asionekane uwanjani muda mrefu, lakini akija kuonekana basi anafanya kitu kimoja kizuri chenye faida kwenye timu, hivyo anastahili kuwepo katika kikosi changu,” amesema Kaze.

 

Kaze aliongeza kuwa, kijana wake huyo huwa anafanya vitu vingi kwa usahihi vile anavyomuelekeza anapokuwa mazoezini ambapo huvihamishia uwanjani jambo ambalo lina faida kwa timu yake.

 

Yanga ipo nafasi ya kwanza ikiwashushusha Azam FC jana, Novemba 25 baada ya ushindi wa bao 1-0 lililopachikwa na Deus Kaseke. Kwenye mchezo huyo kiungo huyo alikuwa benchi akishuhudia balaa la kiungo mzawa Fei Toto na Farid Mussa.

 
That Gal ya Rosa Ree Yawa Gumzo Itazame Hapa chini:

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments