11/08/2020

Mbosso Asimulia Msoto Kuvunjika YamotoSTAA wa muziki wa Bongo Fleva anayekiwasha chini ya Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Mbwana Yusuf ‘Mbosso’ amesimulia msoto aliopitia kwenye maisha yake baada ya kuvunjika kwa Yamoto Band.


Akizungumza na Risasi Vibes, Mbosso amesema, mara baada ya kusambaratika kwa Yamoto, wasanii wenzake walianza kutoa kazi ila kwa upande wake hakuwa na mbele wala nyuma, jambo ambalo lilimfanya aone maisha ya muziki ni magumu.


“Binafsi mimi kipindi Yamoto Band imevunjika, nilipoteza mwelekeo kabisa, sikuwa najua cha kufanya. Kiukweli nilihangaika huku na kule bila mafaniko, ila ninatoa shukrani zangu za dhati kwa meneja wangu, Mkubwa Fella, amenisaidia sana mpaka hapa nlipofikia,” anasema Mbosso.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

1 comment:

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger