Mwanaume afariki ghafla ndani ya basi la umma Kenya

 


Wasafiri waliokuwa wamepanda katika basi la umma katika mji mkuu wa Kenya Nairobi, waliingiwa na hofu, baada ya mwanaume mmoja kufa ghafla ndani ya basi hilo.

Wasafiri na kondakta walitambua kuwa mwanaume huyo amekufa wakati walipojaribu kumuambia atoe njia kwa msafiri mwenzake ambaye alikuwa anataka kutoka ndani ya gari lakini hakuweza kujibu lolote na alionekana kupoteza fahamu.


Maafisa wa wizara ya afya waliitwa katika eneo la tukio baada ya polisi kukataa kusafirisha mwili kwa hofu ya uwezekano kuwa mwanaume huyo alikuwa na maambukizi ya Covid-19.


Maafisa waliupulizia dawa mwili wa mwanaume huyo ulipokuwa ndani ya mwili na baadaye waliondoka nao ndani ya mfuko.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments