Mwigizaji The Rock Ashindwa Kukubali Kuwa Michael B. Jordan Ndio Mwanaume Mwenye Mvuto zaidi Duniani


Muigizaji Dwayne 'The Rock' Johnson kwa utani ameshindwa kukubali matokeo ya ushindi wa Michael B. Jordan kama Mwanaume mwenye mvuto zaidi duniani kwa mujibu wa Jarida la PEOPLE.


Kupitia ukurasa wake wa instagram, The Rock ambaye pia alishinda taji hilo mwaka 2016, aliweka post na kumpongeza Michael B. Jordan kisha akashindwa kukubali matokeo hayo kwa kuandika "I Concede Nothing" msemo ambao pia umetumiwa na Rais Donald Trump baada ya Joe Biden kutangazwa mshindi wa Kiti cha Urais wa Marekani mwaka huu.


Wiki iliyopita, ushindi wa muigizaji huyu maarufu wa filamu ya 'Black Panther' na nyingine kali uliacha maswali mengi kwenye vichwa vya watu, wengi wakihoji kwamba amepatikana kwa vigezo gani.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments