Pompeo akutana na wawakilishi wa Taliban na serikali ya Afghanistan kujadili mchakato wa amani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo, amekutana na wawakilishi wa kundi la Taliban na wajumbe wa serikali ya Afghanistan kwa ajili ya mazungumzo ya mchakato wa amani.

Kulingana na maelezo yaliyotolewa na ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, iliarifiwa kuwa Pompeo alikutana na wawakilishi hao pamoja na mwenyekiti wa idara ya masuala ya kisiasa ya Taliban Molla Birader katika mji mkuu wa Doha nchini Qatar. 

Pompeo pia alikutana na wawakilishi wa Afghanistan na kutoa wito wa kuendeleza mazungumzo ya mchakato wa amani kwa pande zote mbili husika huku akiwapongeza kwa maendeleo yaliyopo.

Pompeo alitaka mizozo ipunguzwe, mwelekeo wa kisiasa uwekwe, suluhisho la kudumu la kusitisha mapigano lipatikane, na kusisitiza kuwa wananchi wa Afghanistan wana haki ya kuishi kwa amani na utulivu baada ya kumwaga damu kwenye vita vinavyoendelea kwa kipindi cha miaka 40 nchini humo.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad