Shule 38 Zafutiwa Matokeo Darasa la Saba, Yasome Hapa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


BARAZA la Mitihani la Tanzania (Necta) limewafutia matokeo watahiniwa 1,059 kutoka shule 38 zilizofanya udanganyifu katika mitihani ya kuhitimu darasa la saba mwaka huu.

 

Akitangaza matokeo hayo leo Jumamosi, Novemba 21, 2020 Jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk Charles Msonde, amesema watahiniwa hao hawatapata nafasi nyingine ya kurudia mitihani hiyo.

 

Alisema pamoja na kamati ya mitihani kutimiza wajibu wao vizuri, kulijitokeza matukio machache ya udanganyifu wa mitihani katika baadhi ya shule nchini.

 

“Jumla ya shule 38 sawa na asilimia 0.22 ya shule zote za msingi 17,329 zilizofanya mitihani, zimebainika kufanya udanganyifu wa mitihani kwa namna mbalimbali. Watahiniwa 1,059 sawa na asilimia 0.1 ya wote 1,023,950 waliofanya mitihani walibainika kudanganya,” amesema.

 

Ameongeza kwamba shule hizo zilifanya makosa mbalimbali ikiwamo kuiba mitihani, kugawa majibu kwa wanafunzi na kubadilisha watahiniwa kwa kuwaweka wasio halisi kuwafanyia mitihani wanafunzi watoto.

 

Shule zilizobainika kufanya udanganyifu huo ni pamoja na Ngiloli, Nguyami, Ibuti, Ihenje, Bwawani, Mogohigwa, Chakwale, Msingisi zilizopo Halmashauri ya Gairo.

 

Zingine ni Mafiri, Kibogoji, Ng’wambe, Digalama, Dihinda kutoka Halmashauri ya Mvomero na shule za msingi za Nyawa A iliyopo Halmashauri ya Bariadi vijijini (Simiyu).


 


Shule zingine ni za Halmashauri ya Chabutwa, Sikonge Tabora ikiwemo shule ya msingi Chabutwa, Usagari, Uyui Tabora Siashimbwe iliyopo Moshi Kilimanjaro, Dominion Arusha, Matogoro ya Tandahimba Mtwara, Ng’arita Bariadi Vijijini mkoani Simiyu, Olkitikiti Kiteto iliyopo Manyara na Nyamimina Buchosa, Mwanza.


 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad