Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Siri Imefichuka...Laptop Yafichua Hujuma Simba...Meseji za Whats App Zabambwa

 


HATIMAYE siri imefi chuka kuwa kompyuta mpakato ‘laptop’ aliyokuwa akiitumia mtendaji mmoja wa Simba ndiyo imeonyesha kuwa timu hiyo inahujumiwa na wapinzani wao.

 

Hivi karibuni Klabu ya Simba iliwatimua watendaji wake wanne, lakini haikuweka wazi sababu rasmi zilizochangia kuwatimua watu hao.

 

Simba iliwatimua Meneja Patrick Rweyemamu, Kocha wa Makipa Muharami Mohammed, Ally Shantra na Jacob ambao wapo kitengo cha habari.

 

Timu hiyo imefanya hivyo baada ya kutoka kupoteza michezo miwili mfululizo kwenye ligi hali iliyozua sintofahamu licha ya kuwa ilifanya usajili mkali kwenye dirisha kubwa lililofungwa Agosti 31, mwaka huu.

 

Awali, Simba ilipokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Prisons kule Sumbawanga katika Uwanja wa Nelson Mandela kisha ikapokea kichapo kama hicho dhidi ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar.

 

Chanzo cha ndani kutoka Simba kimelieleza Championi Jumamosi kuwa, hujuma hizi zilibainika baada ya mtendaji mmoja aliyeondolewa kwenye timu hiyo kukabidhi kompyuta ya ofi si ambayo alikuwa anaitumia ilikuwa na meseji kadhaa za mtandao wa WhatsApp kuonyesha kuwa alikuwa na mawasiliano na kigogo mmoja wa timu pinzani.

 

“Unajua mara nyingi ukitumia WhatsApp kwenye kompyuta lazima uwe makini sana vinginevyo inaweza kukuumbua.

 

“Kuna ofi sa mmoja aliondolewa hapa, lakini kwa kuwa alikuwa anatumia kompyuta ya ofi si alitakiwa kuikabidhi na kwa bahati alikuwa hajafunga WhatsApp yake kwenye kompyuta na hivyo meseji zikawa zinaendelea kuingia zikionyesha jinsi ambavyo amekuwa akiwasiliana na kigogo mmoja mkubwa wa wapinzani.

 

“Meseji zile zilikuwa zinaonyesha jinsi ambavyo kigogo huyo anataka kufahamu baadhi ya mambo ikiwa ni pamoja na kufahamu mambo mengi yanayohusu usajili wa timu na alikuwa anajibiwa na mtendaji huyo lakini pia kulikuwa na meseji za watendaji wengine ambao zilionyesha wakiulizana baadhi ya mambo na mtendaji huyo,” kilisema chanzo hicho.


Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments