Spika Ndugai ''tutaendelea kuwatambua wabunge 19 wa CHADEMA''
SPIKA wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, amesema, Bunge litaendelea kuwatambua wabunge wote walioapishwa wakiwemo 20 kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) 19 wa Viti Maalum na mmoja aliyeshinda katika uchaguzi mkuu.
Ameyasema haya leo Novemba 30 wakati akaiwaapisha wabunge wawili, Humphrey Polepole na Riziki Lulida kwenye viwanja vya Bunge, Dodoma.

''Waliokuwa na wasiwasi kuhusu wale Wabunge 19 (Halima Mdee na wenzake) sijui kuna hili kuna hili, niwatoe wasiwasi wale ni Wabunge kamili, na Wanahabari mkiwaandika muwaite Waheshimiwa”amsema Spika wa Bunge, Job Ndugai

Pia ameongeza kuwa Watanzania tupige vita na tukatae ukandamazaji dhidi ya Wanawake kwenye Jamii yetu kwa kisingizio chochote, Mbowe ni Rafiki yangu amesimama akaanza kuwatukana hadharani Wabunge hawa Wanawake ni aibu kuwatukana Wanawake hadharani”-NDUGAI

“Mbowe umesahau Mdeee alivunjika mkono kwa ajili ya kukufuata Magereza, Bulaya apigwa akazimia amepelekwa Aga Khan kwa ajili yako Mbowe, Matiko amelazwa Segerea mara nyingi kwa ajili yako, mshahara wao kuwafukuza hadharani bila kuwasikiliza, haiwezekani”-

Aidha amesema hivi karibuni atawapanga wabunge katika kamati mbalimbali baada ya rais kuunda baraza la mawaziri.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

1 Comments

 1. exactly, Hawa ni Waheshimiwa Wabunge wwa Jamuhuri ya Muungano. Wataendelea kutumikia kiapo chao mpaka 2025.

  Shukurani ya Punda (Faru Joni) ni Mateke. Baada ya hawa kina
  mama Kukijenga na kuimarisha hii Saccoz.

  Halima, Salome, Ester's na wenzenu wote, Zibeni masikio huyu
  TAPELI MBABAISHAJI amesha piga mahesaabu akishirikiana na Minyikaa , anaona michango iwe 20% na makato mil 2. tatizo mgao baina yao ndio haukupata Muafaka ndio wamejilipua.

  Tafadhalini fungueni RB hapo Jijini Dodoma, huyu mbabaishaji
  ana nia ya Kijinai kulingana na aliyozungumza.

  Tunajua nia na Lengo lake kwa nchi hii (Bila kikomo) pia nia
  ya kusepa anayo na anamtumia Boni Jakobo, sinaUhakika kama
  Mbilinyi amesha sepa nchi au yuko na Ponda Salum mwilimu.

  Mrema is a Gentlemani, ameukataa huu mchongo.

  Kina Mama Oyeee,
  Halima na timu ya Upinzani Oyeee,
  Kina Mama Majasiri, Wachapa kazi, Wajenga Hoja, Wanaojitambua oyeeee...!!!!

  Waheshimiwa Wabunge Matiko, Bulaya, Makamba , Mdee Wasiwababaishe hawa Genge la Wababaishaji, Tumesha anza kujipanga on Mtowe impeachment process . Hatufai kuendelea kuwa Mny Kigoda. Amesha Overstay. Na Ana historia mbaya.

  Tokea kwa aliyo panga na yaliyo watokea, wakiwemo Zwitto,Lizzu ben sanane na wengine wengi.

  Tahadhari na onyo kwake, Ukiwagusa kina mama. Tutalala mbele
  pamoja na wewe. UHUNI WENU SASA BASI , B.JACKO UMESIKIA
  Mateja na Bodaboda hawataki mchezzo huu tena. SAS BASI.

  ReplyDelete