Sugu: Tulia Aachane na SuguAliyekuwa mbunge waJjimbo la Mbeya Mjini, kupitia CHADEMA, Joseph Mbilinyi ‘Sugu‘, amesema yeye hana mamlaka ya kumkabidhi ofisi mbunge wa sasa wa jimbo hilo kupitia CCM, Dkt. Tulia Ackson, kwani ofisi aliyokuwa akiitumia, alikwisharudisha funguo kwa mamlaka husika na kwamba amuache na achape kazi.

 

“Wewe umeshasikia wapi mbunge analia hajakabidhiwa ofisi, hakuna kitu kama hicho, aliyempa cheti cha ubunge ndiye angemwelekeza kwamba kinachofuata ni nini, afanye kazi aachane na Sugu.

 

“Yeye afuate utaratibu pengine hata sasa wamempa ofisi nyingine yeye ni mtu wa kujimwambafai, labda ofisi niliyokuwa naitumia mimi ni ndogo nadhani haitaki anatafuta ‘justification’ wampe ofisi kubwa zaidi kwa kusema Sugu hajanikabidhi ofisi, ofisi ni mali ya jiji,” Sugu.

 

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

1 Comments

 1. Mbilinyi, una nini hasa..??
  Tatizo lako nalijua. Lakini ndiyo chaguo letu. Kaa utulie.

  Tulia yuuko pale Katulia, na hata bungeni yuko Katulia haendi Bonanza.

  Njoo Kilombero tulime shamba lipo au na wewe ndio kama yule alie nanihi...

  TULIA MBILINYI, usiwe SUGU.

  ReplyDelete