Taifa la Scotland limekuwa taifa la kwanza duniani kugawa pedi kwa wanawake bureUskochi limekuwa taifa la kwanza duniani kufanya bidhaa za sodo/pedi kugawiwa bure kwa kila mtu. Wabunge walipitisha mswada huo bila kutoa taarifa siku ya Jumanne.Na sasa mamlaka imetoa idhini kisheria kuhakikisha kuwa bidhaa hizo zinatolewa bure kwa yeyote anayehitaji. Mswada huo ulitmbulishwa na waziri wa ajira bi. Monica Lennon.

Alikuwa anafanya kampeni ya kukomesha umaskini wa kununua bidhaa hizo tangu mwaka 2016.

h
Alisema kuwa ni suala linawezekana kufanyika na sheria tu ndio inaweza kutoa muongozo wa kila kitu na sasa ni muhimu zaidi kutokana na janga la corona.

“Siku za hedhi haziachi kutoka wakati wa janga na kazi kubwa inapaswa kufanywa kuhakikisha pedi au sodo hizo zinatolewa bure,” aliongeza.

Umasikini wa sodo ukoje? Umasikini wa sodo ni pale watu wenye kipato cha chini kushindwa kununua pedi. Boksi moja la pedi zinazoweza kutumika siku tano zina gharama ya paundi 8 na baadhi ya wanawake hawawezi kugharamikia .


 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments