11/22/2020

Takwimu mpya zaonesha COVID-19 imeuwa watu 1,373,381

 


Virusi vya corona vimesababisha vifo vya watu 1,373,381 tangu kuzuka kwake mwezi Desemba huko China. Taarifa hizi ni kwa mujibu wa takwimu kutoka kwenye vyanzo rasmi zilizokusanywa na Shirika la Habari la Ufaransa, AFP. 

Visa vilivyoripotiwa vimefikia 57,583,290 ambapo miongoni mwa hivyo watu 36,725,500 wanatazamwa kamba ndio waliopona. Kulingana na takwimu za jana, duniani kote kuliripotiwa vifo vipya 11,847 na maambukizi 657,054. 

Kwa mujibu wa majumuisho hayo, mataifa yaliyobainika kuwa na vifo vingi vipya ni pamoja na Marekani yenye vifo 1,878, Ufaransa vifo 1,138 na Mexico 719. 

Marekani ambayo imeathirika vibaya na janga hilo, ina jumla ya vifo 254,424 kutoka katika maambukizi 11,913,945. Takriban watu 4,457,930 wameripotiwa kupona virusi vya corona.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger