Uingereza Yatangaza Awamu Mpya Ya ‘Lockdown’

 


WAZIRI Mkuu wa Uingereza Boris Johnson, ametangaza awamu ya pili ya Lockdown kwa muda wa wiki nne hatua hiyi imekuja kama sehemu ya kudhibiti maambukizi pamoja na tahadhari ya kuwa huenda hospitali zitazidiwa wagonjwa ndani ya wiki za hivi karibuni.


Boris amesema sherehe za Krismasi zinaweza kuwa tofauti mwaka huu lakini anaamini kuchukua hatua sasa kunaweza kusaidia familia/ndugu kukusanyika kusherehekea.

 

Katika zuio hili, Baa, Migahawa, sehemu za mazoezi na maduka ya bidhaa zisizo za lazima yatalazimika kufungwa kwa wiki nne kuanzia Alhamisi tarehe 5 Novemba lakini Shule, Vyuo na Vyuo Vikuu zitaendelea kuwa wazi.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE