Watu 50 wapoteza maisha kutokana na ugonjwa usiojulikana Nigeria
Mwanachama wa bunge la Utawala wa eneo la Olamaboro lililoko mkoani Kogi  Ujah Anthony Alewo, alitoa maelezo na kuarifu kufariki kwa watu 50 katika eneo la Etteh kutokana na ugonjwa usiojulikana.


Akibainisha miongoni mwa watu waliofariki kuwa wagonjwa wenye umri wa kati ya miaka 25-40, Alewo alisisitiza kwamba hali hiyo inazidi kutia hofu.


Alewo aliongezea kusema kuwa uchunguzi unaendelezwa ili kubaini chanzo cha vifo. 


Mnamo mwezi uliopita, mikoa ya Delta na Enugu ilikumbwa na janga la ugonjwa usiojulikana ambao baadaye ulifanyiwa uchunguzi na kubainishwa kuwa homa ya manjano. 

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE