Waziri wa Mawasiliano asikitishwa na ubovu wa mashine ya meli ya MV Mapinduzi II

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Waziri wa mawasiliano na uchukuzi, Rahma Kassim Ali amesikitishwa na ubovu  wa mashine ya meli ya MV Mapinduzi II tokea iliponunuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar tokea mwaka 2015.
Hayo ameyasema leowakati alipofanya ziara ya kuzitembelea taasisi zilizomo chini ya wizara yake ikiwa ni agizo kutoka kwa rais alilolitoa wakati  akiwaapisha mawaziri ya kuwataka kuzifahamu taasisi na idara wanazozisimamia .

Amesema anasikitishwa na meli ya MV Mapinzuzi II kushindwa kuendelea kwa shughuli za usafirishaji wa abiria na mizigo kwa muda wa miezi miwili sasa na kila siku meli hiyo inagharimu million nne kwa siku kwa ajili ya mafuta.

Kwa upande wa mhandisi mkuu wa meli hiyo Ramadhan Mwinyi Ramadhan amemthibitishia Waziri kuwa jambo linalopelekea meli hiyo kuharibika mara kwa mara ni kuwa meli hiyo ilinunuliwa na kukabidhiwa ikiwa na mashine mbovu.

Aidha ameutaka uongozi wa shirika la meli kuwasili wizarani  kwa lengo la kukaa pamoja na kuweza kulijadili tatizo hilo ili meli hiyo iweze kufanya safari zake za Unguja na Pemba.

Pia  Waziri huyo amefurahishwa na kasi ya uondoshwaji wa makontena katika bandari kuu ya Zanzibar na kumtaka mkurugenzi wa bandari Bw. Nahat  Mohammed Mahfoudh  kuendelea na kasi hiyo ili kuongeza mapato ya Taifa.

Kwa upande wake  Mkurugenzi wa bandari amesema ili kuendena na kasi ya maendeleo iliyopo ipo haja kwa mamlaka ya bandari kutumia mfumo mpya wa teknolojia wa utowaji mizigo badala ya mfumo wa zamani ili kurahisisha huduma kwa watumiaji wa banadari hiyo.

Wakati huo huo waziri wa mawasiliano na uchukuzi ametoa agizo kwa wakala wa barabara kuhakikisha wanaunda kamati itakayoshughulikia ukarabatiwa barabara zote zenye mashimo kwa kuanza na barabara ya uwanja wa ndege ambayo imekuwa ikileta taswira mbaya ya mji wa Zanzibar.

Sambamba na hilo alisisitiza wafanyakazi wa wakala wa barabara kupatiwa stahiki zao wanazostahiki  ili wafanyakazi hao wafanye kazi kwa ufanisi.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mama, we needto go One step further,
    ikiwemo kurudia mchakato wa manunuzi na ukabithiwaji. unawawajibisha wote.

    Badilisha Wakurugenzi na Bodi zao haraka Ikihitaji kufanya hivyo ktk System na kuondoa mtandao wa Wahujumu

    Kuwa mkali khasa kwenye Ubadhirifu.
    Mwinyi anataka wasaidizi wanaojielewa na kumuelewa.

    Tusionneane Muhali wala Staha.

    Ni Kazi iliyo tukuka kwenda Mbele.

    Yajayo ni Neema Tupu. Hapa Kazi tu.

    ReplyDelete

Top Post Ad