Anthony Joshua amjibu Tyson FuryBaada ya bondia wa Uingereza Anthony Joshua anayemiliki mikanda ya IBF, WBA na WBO, kufanikiwa kuitetea kwa kumpiga kwa KO raundi ya 9 Mbulgaria Kubrat Pulev, bingwa wa dunia wa WBC Tyson Fury amejitokeza na kudai atampiga Joshua ndani ya raundi tatu.

Tyson Fury amesema, ''nataka kupigana na Joshua, nimpige ndani ya raundi tatu na nadhani nitamwonesha ubora mkubwa uliopo ndani yangu''.


Hata hivyo bondia wa Uingereza Anthony Joshua mwenye miaka 31, amemjibu Fury kwa kusema, ''imekuwa vizuri kama anataka kupigana, ni habari njema angalau sasa naweza kuwa na uhakika wa kukutana naye uliongoni''.


Pambano hilo ambalo linatajwa kuwa huenda likafanyika mwezi Machi mwaka 2020, litakuwa ni pambano la kwanza kuwakutanisha mabondia wanaomiliki mikanda yote ya uzito wa juu ambayo ni IBF, WBA na WBO kwa Joshua na WBC kwa Tyson Fury.


Usiku wa kuamkia leo Desemba 13, 2020, kwenye uwanja wa Wembley nchini Uingereza, Anthony Joshua alimpiga kwa KO raundi ya 9 Mbulgaria Kubrat Pulev.


 


KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLO

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments