Familia Wagombania Mali za Maradona

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




ATAENDELEA kukumbukwa kuwa ni shujaa wa soka, ikiwemo mafanikio yake katika Kombe la Dunia 1986 alipofunga bao la ‘Mkono wa Mungu’ dhidi ya England, lakini upande wa pili familia yake inaweza kumkumbuka tofauti.

 

Huyo ni Diego Mara dona ambaye alifariki wiki kadhaa zilizopita ameacha vita kubwa ya urithi wa mali zake hasa kwa watoto.

 

Inaelezwa kuwa licha ya watoto sita ambao wanajulikana bado kuna wengine ambao wameibuka na kuhusu mgawanyo wa mali za Maradona umeanza kuwa tatizo.



Inaelezwa kuwa Maradona ameacha utajiri wenye thamani ya pauni 37m na katika waraka aliouandika wa jinsi mali zake zitakavyo gawanywa hapo ndipo kumeibuka na kizaazaa.

 

Watoto wanao julikana na wengi kuwa ni wa staa huyo ni watano, lakini kuna mwingine ameibuka, kuna dada zake wanne na wapenzi wake na wake zake wa zamani nao wametajwa kutaka kuwemo katika urithi huo.

 

Wanasheria wa familia ya Maradona wanatarajiwa kuanza kuingia katika vita ya mgawanyo wa mali kwa kuwa wapo ambao wanaona walistahili kupata nyingi au kiasi kikubwa kuliko wengine na wapo wanaoona kuwa wote wanatakiwa kupewa mgao sawa kama marehemu mwenyewe alivyotaka iwe.

 

Watoto maarufu wa nguli huo, Dalma, 33, na Giannina, 31, wamekuja juu na kumshutumu mwanasheria wa Maradona, Matias Morla, ambaye ndiye aliyeweka wazi juu ya waraka wa Maradona aliouandika mwaka 2012, wakidai kuwa anahusika katika mambo mbalimbali ya ‘kipuuzi’ kuhusu urithi wa baba yao.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad