FIFA yamfungulia mashtaka ya makosa ya jinai aliyekuwa Rais wa shirikisho hilo Sepp Blatter

 


 Shirikisho la soka duniani (FIFA) limefungua mashtaka ya makosa ya jinai dhidi ya aliyekuwa Rais wa shirikisho hilo Sepp Blatter.

Blatter na kampuni kadhaa wanatuhumiwa kuliingiza shirikisho hilo la soka duniani kwenye hasara kufuatia kuingia mkataba wa maboresho ya makumbusho ya shirikisho hilo sambamba na kukodishwa kwa ofisi 34 kwa mkataba wa £267.8m (zaidi ya Shilingi bilioni 750).


Mkataba huo wa upangishwaji wa ofisi ulianza mwaka 2016 na utaisha mwaka 2045.


Makumbusho hayo yaliyopo Zurich nchini Uswisi yalijengwa miaka ya 1970 na yalifanyiwa ukarabati kwa £104.2m (Zaidi ya Shilingi bilioni 290) na kufunguliwa tena mwaka 2016.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments