Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Kina Mdee wadaiwa kuandaa kongamano Bawacha, mwenyewe akanusha

 Dar es Salaam. Wabunge 19 wa viti maalumu waliofukuzwa Chadema, wanadaiwa kuandaa kongamano la wanawake kinyume na maelekezo ya chama hicho ya kuwakataza kutoshiriki shughuli zozote za chama.


Wabunge hao wanaoongozwa na Halima Mdee aliyekuwa mwenyekiti wa Baraza la Wanawake (Bawacha) walifukuzwa uanachama Novemba 27, baada ya kwenda bungeni jijini Dodoma kuapishwa bila kufuata utaratibu wa chama hicho.


Kulingana na taaarifa iliyotolewa jana na makamu mwenyekiti Bawacha Zanzibar, Sharifa Suleiman, wabunge hao 19 wamewapigia simu wanawake wa baraza hilo wakiwashawishi kushiriki kwenye kongamano hilo ambalo halikuwekwa wazi litafanyika lini.


Alisema chama chake hakijaandaa kongamano hilo la wanawake, ila Mdee na wenzake wanataka kuwashawishi wanawake wa Chadema washiriki ikiwa ni kutafuta jukwaa la kuonyesha kuwa wanaungwa mkono.


“Tumepata taarifa wanatumia nembo na jina la Chadema kuwahadaa baadhi ya viongozi na kina mama wa Bawacha kwa fedha na ahadi za mitaji ya biashara na mafunzo ili wafike Dar es Salaam kwenye kongamano.


“Mwanachama yeyote atakayeshirikiana na watu hawa 19 atambue atakuwa anakiuka taratibu na maamuzi ya chama na atachukuliwa hatua stahiki kwa mujibu wa katiba ya chama cha mwongozo wa Bawacha,” alisema Sharifa.


 Makamu mwenyekiti huyo aliongeza kuwa mbali na kuendelea kufuatilia nyendo za Mdee na wenzake, baraza hilo limewataka wajumbe wake kuwa imara wakati wanaendelea kujipanga kutekeleza maagizo ya kamati kuu ya kuziba pengo la hao 19 waliovuliwa uanachama.


Akizungumza na gazeti hili, Mdee alikanusha kuhusu taarifa hiyo na kuwataka wanawake wa Bawacha kujikita kwenye kujenga chama na kuachana na majungu. “Mimi kwa sasa nashughulika na rufaa ya Baraza kuu, hizi habari za kuokoteza sina muda wa kuzifanyia kazi, ni habari za uzushi. Sisi tumeheshimu uamuzi wa chama, tuko kwenye muda wa rufaa.


“Kama nikitaka kufanya shughuli za kijamii sishindwi. Nawashauri viongozi wa Bawacha waliobaki walijenge baraza ambalo sisi tulipambana kujijenga mpaka limepata heshima, waachane na Mdee,” alisema Mdee.


Alisema maelekezo ya chama yalikuwa wazi kwao kwamba wasifanye shughuli za chama na yeye kwa sasa si mwenyekiti, bali ni mwananchi wa kawaida.


Kuhusu muda wa rufaa alisema: “Bado tuko ndani ya muda wa rufaa. Katiba ya Chadema inasema siku 30 baada ya kupata taarifa ya maandishi. Tulipata taarifa Novemba 30, ikifika Desemba 29 ndiyo mwisho, ndipo mtuulize.”


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

6 Comments

 1. Mheshimiwa Mdee na Waheshiwa wabunge kina Mama Wajasiri na Wazalendo, mmejikuta katika wimbi la Mizengwe la mfumo Dume ambao unajinasibisha na kujigamba kwamba hata viti vya kina mama haki yao sisi ndio waamuzi. Tunasema HAIWEZEKANI TUKO KARNE YA 21 FOR WOMENS EMPOWERMENT. Kina mama ukiwemo wewe Sharifa, emancipate from the long tenuture of Mbowe kukosa imani nae katika uongozi wake wa ki imla na uchakachuaji wa RUZUKU NA UKUSANYAJI WA KINACHOITWA MICHANGO YA MAGUMASHI.

  WAKE UP ALL BAWACHA UNITE FOR YR RIGHT.

  Waheshimiwa Wabunge need to impeach mwenyekiti Mh Cecil Mwambe was Right. Mbweo anahitaji kupumzishwa.

  KINA MAMACAN DO THAT. TUKO PAMOJA.

  ReplyDelete
  Replies
  1. Hivyo kile kikao kilikuwa halali na Mwinyi Kaa alikidhi vigezo na Masharti mpaka kuhatarisha Amani na Usalama Wa Waheshimiwa Wabunge..??

   Nnavyo jua mie baadhi ya waliohudhuria hawana sifa kwa namna moja au nyingine. hence azma/Uamuzi ni Batili

   Delete
 2. Maalim Seif Na Zitto... Oyeeeee
  Wazalendo na Wakereketwa...Oyeeee
  Bawachadema.....Oooyyyyeee....oyeee

  Mheshimiwa Mdee na Waheshiwa wabunge kina Mama Wajasiri na Wazalendo, mmejikuta katikati ya wimbi la Mizengwe la mfumo Dume ambao unajinasibisha na kujigamba kwamba hata viti vya kina mama haki yao sisi ndio waamuzi. Tunasema HAIWEZEKANI TUKO KARNE YA 21 FOR WOMENS EMPOWERMENT. Kina mama ukiwemo wewe Sharifa, emancipate from the long tenature of Mbowe kukosa imani nae katika uongozi wake wa ki Imla'a na uchakachuaji wa RUZUKU NA UKUSANYAJI WA KINACHOITWA MICHANGO YA MAGUMASHI. (Mchongo wa Ulaji Kinyemela)

  WAKE UP ALL BAWACHA UNITE FOR YOUR RIGHT. TIME IS NOW.

  HE DID THIS TO Mh.KITILA MKUMBO, ZITTO NA WENGINE EARLIER

  Waheshimiwa Wabunge need to impeach mwenyekiti.
  Mh Cecil Mwambe was Right. Mbweo anahitaji kupumzishwa.

  KINA MAMA CAN DO THAT. TUKO PAMOJA.

  ReplyDelete
  Replies
  1. Hivyo inaigia akilini..? Mh Bulaya/Matiko/Mdee/Kunti/ Agnesta,Hanje,Sharifa ,Makambana Kina Bawacha wote
   wajenge taasisi hii, halafu kiurahisi uwatolee nje.

   KWELI JAMENI..!!!???

   UTATOKA WEWE. TENA NASEMA, **UTATOKA WEWEEEEE**

   HAIWEZEKANI..!!! Kama si wewe, BASI NI NYINYI .

   PIGA KELELE KWA MAMA'KEEEE. KINA MAMA JEMBEEEE.!!!

   Delete
 3. FARU JONI NA USANII...OYEEE
  UHAMASISHAJI WA VIBEKO ...MAANDAMANO..PWA PWA..PWAAAA..!!!

  Maalim Seif Na Zitto... Oyeeeee
  Wazalendo na Wakereketwa...Oyeeee
  Bawachadema.....Oooyyyyeee....oyeee

  Mheshimiwa Mdee na Waheshiwa wabunge kina Mama Wajasiri na Wazalendo, mmejikuta katikati ya wimbi la Mizengwe la mfumo Dume ambao unajinasibisha na kujigamba kwamba hata viti vya kina mama haki yao sisi ndio waamuzi. Tunasema HAIWEZEKANI TUKO KARNE YA 21 FOR WOMENS EMPOWERMENT. Kina mama ukiwemo wewe Sharifa, emancipate from the long tenature of Mbowe kukosa imani nae katika uongozi wake wa ki Imla'a na uchakachuaji wa RUZUKU NA UKUSANYAJI WA KINACHOITWA MICHANGO YA MAGUMASHI. (Mchongo wa Ulaji Kinyemela)

  WAKE UP ALL BAWACHA UNITE FOR YOUR RIGHT. TIME IS NOW.

  HE DID THIS TO Mh.KITILA MKUMBO, ZITTO NA WENGINE EARLIER

  Waheshimiwa Wabunge need to impeach mwenyekiti.
  Mh Cecil Mwambe was Right. Mbweo anahitaji kupumzishwa.

  KINA MAMA CAN DO THAT. TUKO PAMOJA.

  ReplyDelete
  Replies
  1. Kama ni mbwai na iwe mbwai.
   ilikuwa ACT Tanzania na ACT Wazaendo.

   Sasa, Cha Ajabu nini..!!?

   Sitto si Yule yule..!! Mbweo IMEKULA KWAKO!! BIG TIME

   Delete
Emoji
(y)
:)
:(
hihi
:-)
:D
=D
:-d
;(
;-(
@-)
:P
:o
:>)
(o)
:p
(p)
:-s
(m)
8-)
:-t
:-b
b-(
:-#
=p~
x-)
(k)