Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Meja Kunta Ajilipua Penzi La Malkia KarenVUNJA ukimya! Staa wa Singeli, Khalid Sadick ‘Meja Kunta’ kwa mara ya kwanza ameamua kujilipua na kuanika uhusiano wake wa kimapenzi na msanii wa Bongo Fleva, Karen Habash ‘Malkia Karen’.

Meja amefunguka hayo ikiwa ni baada ya madai kufukuta chini kwa chini na watoto wa mjini kushindwa kuwa na uhakika wa moja kwa moja kama kweli ni wapenzi au la.

 

Akizungumza na AMANI, Meja Kunta amesema mahusiano yao yalianza hata kabla ya kutoa kazi ya pamoja.Aliongeza kuwa, hamasa ya kuwa pamoja katika mahusiano yao ya kimapenzi wameipata pia kutoka kwa wasanii wenzao wa kundi la Navy Kenzo, Aika na Nahreel.“

 

Mimi na Karen sasa ni rasmi sasa tupo kwenye mahusiano, hata watu wanaona jinsi gani tunavyofurahia maisha, najua watu walidhani kwamba ni muziki pekee lakini sasa tumeamua kuweka wazi hisia zetu mitandaoni.“

 

Mahusiano yalikuwepo hata kabla ya kazi, ila tumeamua kutoa kazi ya pamoja, kwa sababu wote ni wasanii hata Navy Kenzo wanafanya hivyo,” alisema Meja Kunta ambaye hivi karibu walitoa ngoma iitwayo Sina.Alipotafutwa Karen ili kuweza kumsikia anazungumziaje ishu hiyo, aliombwa atafutwe baadaye kwa kuwa eneo alilokuwepo alikuwa na watu hivyo hakuweza kulizungumzia.

 

Haika na Nahreel ambao ndio wanawavutia Meja na Malkia, wapo kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa zaidi ya miaka 10 na wamefanikiwa kupata watoto wawili wa kiume.Mbali na mafanikio ya kimuziki, wasanii hao wamefanikiwa pia kwa upande wa maisha binafsi kwani wamejenga nyumba yao ya thamani kutokana na muziki


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments