Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Mlinzi wa Bobi Wine Adaiwa Kufa kwa Kugongwa Gari la JeshiRIPOTI za vyombo vya habari nchini Uganda zimesema kuwa, baadhi ya mashahidi wameripoti kwamba mlinzi wa mgombea urais kupitia National Union Party (NUP), Robert Kyagulanyi Ssentamu ‘Bobi Wine’ aitwaye Francis Kalibala, aligongwa na gari la Jeshi la Uganda (UPDF) wakati msafara wa Bobi Wine upolikuwa unarudi Kampala kutoka Masaka.

 

Katika taarifa yake, Bobi Wine amesema, “Nasikitika kutangaza kifo cha mmoja wa walinzi wangu, Francis Kalibala, aliyegongwa na gari la jeshi, namba H4DF 2382 ambalo liliziba njia karibu na Busega na kutuzuia kupita.”


Msemaji wa Jeshi la Uganda, Brig. Flavia Byekwaso amesema, Francis alianguka kutoka kwenye gari lililokuwa linaendeshwa kwa mwendokasi.


Kabla ya tukio hilo, waandishi kadhaa wa habari walishambuliwa na polisi na kujeruhiwa vibaya akiwemo mpiga picha Ashraf Kasirye wa televisheni ya Bobi Wine ya Ghetto TV, na mwandishi wa Shirika la Habari la Nation Media Group – NTV, Ali Mivule.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments