Museveni Amteua Mwanaye Kuwa Mkuu wa Ulinzi

 


RAIS wa Uganda, Yoweri Museven,i ambaye pia ni amiri jeshi mkuu, amefanya mabadiliko katika jeshi la Uganda (UPDF) na kumrejesha mwanaye Lt-Jenerali Muhoozi Kainerugaba kuwa mkuu wa kikosi cha ulinzi wa rais yaani Special Force Command (SFC).

Mabadiliko hayo yamefanyika wakati wanasisa wa upinzani wakilaumu jeshi la polisi kwa kuwasumbua katika kampeni zao za uchaguzi zinazoendelea nchini humo.

 Muhoozi amerudishwa kwenye cheo ambacho aliwahi kukitumikia kabla ya kubadilishwa kuwa mshauri wa  Museveni katika masuala ya ulinzi na kitengo hicho ndicho kinahusika na kumlinda rais wa Uganda.

Mabadiliko haya yamefanyika wakati kampeni za uchaguzi mkuu wa rais zikiendelea ambapo wanasiasa wa upinzani wamekuwa wakituhumu jeshi la polisi kuwatatiza kwenye kampeni zao, lakini msemaji wa jeshi amesema hayo ni mabadiliko ya kawaida tu.

That Gal ya Rosa Ree Yawa Gumzo Itazame Hapa chini:

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments