Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Nini Amchokoza Mke Mwenzake Kwa Nay Wa Mitego

 
Msanii Official Nini amesema kwa sasa hayupo tena kwenye mahusiano na boss wake Nay wa Mitego, ila huwa ana-post picha akiwa naye kwa sababu hutaka kumrusha roho mwanamke mpya wa Nay wa Mitego.

 

Official Nini ambaye yupo chini ya lebo ya 'Free Nation' inayomilikiwa na Nay Wa Mitego amesema mapenzi yao yameisha muda mrefu sana na kwa sasa kinachoendela ni kumsimamia kwenye upande wa kazi.


"Ile picha ilikuwa ni ya muda mrefu nilijisikia tu kumchokoza wifi, mimi sina mke mwenzangu maana naogopa nisije nikaribu ndoa za watu, yule wa sasa hivi ni wifi yangu kwa boss wangu siku nikikutana naye nitamwambia ampende sana boss wangu hicho ndicho kikubwa" amesema Nini 

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments