Nyota Wanne Yanga Wawania Tuzo ya Mchezaji Bora Novemba

 


NYOTA wanne wa Klabu ya Yanga wanapambania tuzo ya mchezaji bora kwa mwezi Novemba ambao umekamilika jana.

Ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Cedric Kaze ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 31 baada ya kucheza mechi 13.

Wachezaji hao wanaowania tuzo hiyo ni pamoja na kipa namba moja Metacha Mnata ambaye amecheza jumla ya mechi 12 kati ya 13 na beki chipukizi, Bakari Mwamnyeto.

Pia yupo kiraka Deus Kaseke ambaye amefunga jumla ya mabao mawili kwenye mechi mbili mfululizo ilikuwa mbele ya Azam FC na JKT Tanzania.

Mshambuliaji mwenye spidi ila hana bahati ya kufunga naye yumo kwenye orodha hiyo ambaye ni Yacouba Songne mwenye bao moja na pasi mbili za mabao.

Ili kumpigia kura mchezaji unayempenda, Yanga wameweka utaratibu kwamba unampigia kura kupitia akaunti yao ya Twitter,'yangasc1935'.

That Gal ya Rosa Ree Yawa Gumzo Itazame Hapa chini:

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments