Paula na Baba’ake Hapatoshi, Amtetea Mama Yake
MOJA kati ya habari ambazo zimeshika vichwa vingi vya habari wiki hii ni pamoja na mtoto wa staa wa Bongo Movie Kajala Masanja, Paula Paul, kujibizana na baba yake mzazi Paul Matthysse ‘P Funk’ mtandaoni.

 

Ishu ilianzia pale ambapo P Funk alifanya mahojiano na moja ya vyombo vya habari nchini nakusema kwamba binti yake huyo amemshinda kutokana na tabia zake kuwa sio nzuri, hivyo kila kitu ambacho kitatokea kwa mwanaye huyo basi aulizwe mama yake.Kauli hiyo ilionyesha kumkwaza binti huyo nakuamua kuandika walaka mzito katika akaunti yake ya instagram huku akisindikiza na picha ya mama yake.“

 

Hakuna mama bora kwangu kumshinda mama yangu Kajala, kwa sababu umepambana sana kwa mvua na jua ili kunilinda na mabaya na pia kuhakikisha mwanao nakuwa katika mstari mzuri na maisha mazuri, “ haya ni baadhi ya maneno aliyoandika Paula nakuongeza kuwa “ Akinipenda mama yangu inatosha”.
 

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments