Putin akanusha kuhusika katika tukio la kupewa sumu Navalny
Rais Vladimir Putin wa Urusi amesema ripoti za uchunguzi katika vyombo vya habari, ambazo ziliwahusisha maafisa wa usalama wa Urusi na jaribio la kumuuwa kwa sumu mpinzani mashuhuri wa kiongozi huyo, Alexei Navalny, zilikuwa mbinu ya kuwashambulia viongozi wa Urusi. 
Akizungumza jana katika kikao cha kila mwaka cha waandishi wa habari kinachorushwa moja kwa moja kupitia televisheni, Putin alisema kama serikali ingedhamiria kumuuwa mwanasiasa huyo wa upinzani hivi sasa angekuwa marehemu. 

Navalny aliugua ghafla akisafiri kwa ndege tarehe 20 Agosti mwaka huu, na alisafirishwa siku mbili baadaye akiwa bila fahamu hadi Ujerumani alikopatiwa matibabu. 

Shirika la kudhibiti silaha za kemikali lilitangaza kuwa aliwekewa sumu aina ya Novichok iliyotengenezwa enzi ya Muungano wa Kisovieti. 

Mwanzoni mwa wiki hii, makundi mawili ya uchunguzi ya Bellingcat na The Insider, yalichapisha ripoti iliyodai kuwa makachero wa Shirika la Upelelezi la Urusi (FSB) wamekuwa wakimfuata Navalny katika safari zake tangu mwaka 2017.


That Gal ya Rosa Ree Yawa Gumzo Itazame Hapa chini:

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments