Penzi la Fahyma, Rayvanny Limenoga
MZAZI mwenza wa staa wa Bongo Fleva, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ Faima Msenga ‘Fahyma’ amefunguka namna ambavyo penzi lao kwa sasa limenoga.

 

Fahyma amesema kuwa, hayupo tayari kumuacha mumewe huyo kwani wametoka mbali.

 

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA WIKIENDA, Fahyma ambaye ni mwanamitindo maarufu Bongo anasema kuwa, aliacha kunyonya ziwa la mama yake, lakini siyo rahisi kuachana na Rayvanny hivyo manyakunyaku wakae mbali na penzi lao.“Kuna watu wanatamani mimi na Rayvanny tuachane, lakini hilo haliwezekani kwa sababu binafsi nilifanikiwa kuacha ziwa la mama yangu, lakini siyo kumuacha mume wangu (Rayvanny), kwa hiyo ninawapa pole sana kwani ndiyo kwanza mambo yetu yamenoga, wakati wao wanapiga majungu, sisi huku tunainjoi kwa kwenda mbele,” anasema Fahyma.

 

Penzi la Fahyma na Rayvanny ambao wamejaaliwa mtoto mmoja wa kiume aitwaye Jaydenny limepita kwenye misukosuko mingi ambapo kuna wakati linaelezwa kuzimika kabisa kabla ya hivi karibuni kuanza kung’ara tena.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments