Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Simba Kamili Gado Kuwavaa FC Platinum Leo


SVEN Vandenbroeck,Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba amesema kuwa kikosi kipo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe.


Simba itashuka Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe majira ya saa 9:00  alasiri kwa saa za Zimbabwe ikiwa ni sawa na saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.


Mchezo wa leo ni wa hatua ya kwanza ndani ya Ligi ya Mabingwa Afrika na ule wa marudio unatarajiwa kuchezwa kati ya Januari 5-6 2021 Uwanja wa Mkapa.


Kocha huyo raia wa Ubelgiji amesema:"Maandalizi na kila kitu kuhusu mchezo kipo sawa na matumaini yetu ni kuona kwamba tunapata matokeo chanya kwenye mchezo wetu.


 "Tunatambua kwamba mchezo utakuwa mgumu ila tutahakikisha tunapambana kupata matokeo chanya. Kikubwa ambacho tunahitaji ni ushindi na kila kitu tunaamini kitakuwa sawa."


Simba iliweka kambi nchini Zimbabwe Desemba 18 na iliweza kupokelewa na Serikali ya Tanzania kupitia kwa balozi aliyepo Zimbabwe, Profesa Emmanuel Mbennah.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments