Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Simba Kuwakosa Watano Leo Kimataifa

 


SIMBA leo Desemba 23 ikiwa na kazi ya kusaka ushindi mbele ya FC Platinum ya Zimbabwe kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya kwanza itawakosa nyota wake watano.

Nyota hao ni pamoja na :-Bernard Morrison yeye yupo Bongo akiendelea kupata matibabu kwa kuwa hakuwa fiti kiafya. Charlse Ilanfya pia yupo Bongo akiendelea na programu ambayo amepewa na Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck.

Kipa namba moja Aishi Manula yeye alikaa langoni kwenye mechi mbili zilizopita za kimataifa dhidi ya Plateau United anasumbuliwa na majeraha baada ya kuumia kwenye mchezo dhidi ya KMC, Uwanja wa Mkapa. 

Kwenye mchezo huo wa Ligi Kuu Bara alitumia dakika 45 wakati Simba ikishinda bao 1-0 lililofungwa kwa mkwaju wa penalti na Meddie Kagere.

John Bocco nahodha wa Simba naye pia aliumia kwenye mchezo dhidi ya KMC ulikuwa ni wa Ligi Kuu Bara. Kwa mujibu wa Kocha Mkuu, Vandenbroeck hawa watakosekana kwenye mchezo wa leo.

Thadeo Lwanga, ingizo jipya ndani ya Simba, kwa mujibu wa Barbara Gonzalez ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Simba alisema kuwa kumekuwa na ugumu wa kupata vibali vyake

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments