Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Six Packs Haziwezi Kukufanya UKAWA Mwanaume Bora Kitandani

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

 


Maneno mazuri yanaweza kuwa tiba kubwa mbele ya moyo uliokata tamaa. Utamu wa maneno na tungo za ushawishi unavyozipandikiza kinywani mwako vinaweza kumlainisha mwanamke mgumu ambae ameathirika na maumivu ya mahusiano na akawa mwepesi kukuelewa.

Wanawake siku hizi wamekuwa waoga sana kuamini mwanaume kwasababu wanaume wengi siku hizi wamekuwa sio wakweli. Wanaume wengi wamekuwa mario. Mario ni mwanaume asietaka kazi wala hana juhudi zozote za maisha yeye kazi yake ni kumtegemea mwanamke kwa kila kitu.

Mario kazi yake kushinda (GYM) kwa hela ya mwanamke akitafuta mwili wenye mvuto wa kimapenzi ili aendele kuwapagawisha wanawake wa mjini wanaumwa na mapenzi ya six pack. Mwanaume kamili ni yule anaejituma kwa jitihada kubwa ili ahakikishe kuwa mke na watoto wake wanapata mahitaji muhimu.

Maisha ya kuvizia wanawake wenye kipato ili uoe upate chaka la kufichia matatizo yako hayawezi kukunufaisha hata siku moja. Ubora wa mwanaume ni kutafuta usiku na mchana ili jamii yake inayomzunguka iponye majeraha ya changamoto wanazozipitia na sio kukaa ukavizia wanawake wenye hela utumie hela zao.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments