Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Staa wa muziki kutoka Kenya Willy Paul Amshukia Vikali Erick Omondi Kwa Kutumia Nyimbo za Diamond Platnumz Katika Vichekesho vyake

 


Staa wa muziki kutoka Kenya, @willy.paul.msafi ameshindwa kuvumilia suala la mchekeshaji #ErickOmondi kupenda kutumia nyimbo za wasanii wa Tanzania katika video za vichekesho vyake kuliko za Wakenya ambapo amemuomba mchekeshaji huyo aanze kucheza na za kwao.


#WillyPaul amefunguka hayo kwa kuweka comment kwenye clip ya Erick Omondi ambayo alipost kwenye ukurasa wake wa #Instagram akicheza wimbo wa #Diamond, "Yope Remix" ambapo aliandika, "My brother Erico, the president of comedy Africa @ericomondi we have dope songs out here manze... tumia zetu pia. Ama namna gani baba?"


Mara baada ya #WillyPaul kutoa ya moyoni nae Erick Omondi hakusita kuijibu koment hiyo,  "Sawaaa bro, I promise kuanzia sahii ntazitumia Sana"


Kwa mara kadhaa msanii @willy.Paul.Msafi amekuwa akipigania muziki wa Kenya kwa kuhakikisha unapewa nafasi nchini Kenya ambapo siku kadhaa zilizopita alilalamika wasanii wa nchini humo kutopeana sapoti kwenye kazi jambo linalodidimiza kazi zao na kufanya kazi za mataifa mengine kama Tanzania na Nigeria zitawale zaidi.

Tazama Video Mpya ya Rosa Ree -That Gal


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments