Suarez Asababisha Wafanyakazi Wanne wa Chuo Kusimamishwa Kazi, Wamfaulisha Mtihani Wakati Hajui Kitu

 


Mshambuliaji wa kimataifa wa Uruguay Luis Suarez amewaponza wafanyakazi 4 wa chuo kikuu cha Perugia nchini Italia, ambao wanashukiwa kuhusika katika udanganyifu wa Suarez kufaulu mtihani wa lugha ya kiitaliano na kupata B1 wakati hajui lugha hiyo.


Luis Suarez baada ya mambo kuwa magumu FC Barcelona alikuwa anataka kuhamia Juventus ya Italia lakini walikuwa washamaliza nafasi za kusajili wachezaji wanaotoka nje za nchi za jumuiya ya umoja wa Ulaya.
Suarez ndipo akalazimika kuomba uraia wa Italia na kutakiwa kufanya mtihani lakini inaonekana kama alidanganya kwani hajui hata kidogo kiitaliano na inasemekana alikuwa nao mtihani siku moja kabla licha ya kufaulu mpango wake ukakwama na kuhamia Atletico Madrid.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments