Zari Ajuta Kumletea Mondi Watoto
UKIACHANA na zile hekaheka za mama la mama Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kuwaleta watoto Bongo na kujiachia na baba yao, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, taarifa zilizonaswa na AMANI zinaeleza kuwa mwanamke huyo wa Kiganda anajutia safari yake hiyo.

 

TUJIUNGE NA CHANZO

Mtoa taarifa makini kutoka ndani ya familia ndiye aliyeshusha ubuyu huo wa motomoto na kueleza kwamba, pamoja na mambo mengine, Zari alitegemea pengine Diamond Platnumz au Mondi angelegeza ‘kamba’ na kurejesha penzi lao lakini matokeo yake mambo yalikuwa tofauti.

 

“Iko hivi, si unakumbuka ile safari ya Zari na wanaye Tiffah na Nillan hivi karibuni? Ile ilikuwa ni mpango mkakati tu kwamba watoto wanakuja kwa baba yao lakini Zari alijua inaweza kuwa nafasi nzuri ya kurejesha penzi lao ambalo lilikuwa limekufa kwa takriban miaka mitatu sasa,” alisema mtoa taarifa huyo.ALICHOKIKUTA

Mtoa taarifa huyo alizidi kuweka wazi kuwa, Diamond hakuwa na mawazo kabisa na ishu ya mapenzi hivyo hata walipoishi kwenye nyumba yake iliyopo maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar es Salaam, hawakushirikiana kwa lolote zaidi ya kulea watoto (co-parenting).

 

“Mondi alikaza kwelikweli si unajua mtoto wa kike akiamua lake ni lazima liwezekane? Sasa safari hii Mondi kaamua kwelikweli kuweka ngumu, hakutaka kabisa ukaribu ule ambao ungeweza kuhatarisha msimamo wake.

 

WALALA VYUMBA TOFAUTI

“Yaani unaambiwa Mondi aliamua kabisa kuwapa chumba kingine Zari na watoto walale na yeye akawa analala chumba kingine kuepuka mambo yasiwe mengi maana usiku mrefu halafu ulale na mtu ambaye mlishaishi pamoja hadi mkazaa watoto wawili si ni sawasawa na kugusanisha sumaku hasi na chanya halafu utegemee zisinase,” alisema.

 

ZARI ALIA

Mtoa taarifa huyo alisema baada ya Mondi kukaza kwa siku kadhaa ambazo Zari alikaa hapa nchini, kuna siku bibie alijikuta akiaangua kilio peke yake chumbani na baada ya hapo aliamua kuondoka zake kurejea Sauz kwenye makazi yake.

 

“Bibie hiyo siku alijifungia ndani akalia weee sasa baada ya kuona Mondi hasomeki licha ya kumtega kwa mapozi kama yote ndipo akaamua kujiondokea zake,” alisema mtoa taarifa huyo.ZARI ANASEMAJE?

AMANI lilijaribu kumtafuta bibie Zari mwenye pesa zake Sauz ili kusikia anazungumziaje taarifa hizo zilizonaswa kutoka ndani kabisa ya familia lakini bahati mbaya hakuweza kupatikana.

 

KILICHOMPA UJASIRI

AMANI limeelezwa kuwa, kilichompa ujasiri Mondi hadi kuamua kujiepusha na mtego wa Zari ni kwa sanabu tayari alikuwa ameshajiseti kwa ajili ya kufunga ndoa na mpenzi wake aliyekuwa ameshapanga kumuoa.

 

AMANI linafahamu mrembo huyo alikuwa akifanya kazi pande za Uarabuni na tayari alishatua nchini kwa ajili ya jambo hilo baada ya kuamua kuacha kazi nchini humo ili aje kukamilisha mipango hiyo ya ndoa kwani alikuwa ndiye kipenzi cha mama Mondi, Sanura Kassim ‘Sandra’.Hata hivyo, mrembo huyo wa Uarabuni naye baadaye alijikuta akiambulia patupu baada ya Mondi kubadili gia angani kwa kifaa kipya ambacho bado hakijanaswa sawia kwenye rada za gazeti hili la AMANI.

Kwa sasa Mondi anaelezwa kuwa yupo kwenye mahusiano na kifaa kipya lakini si kati ya wale wote aliozaa nao; Zari, Hamisa Mobeto na Tanasha Donna.

 

Mondi na Zari waliachana rasmi Februari 14, 2018 baada ya bibie huyo kuandika sababu za kuachana kwao kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa ni pamoja na Mondi kuchepuka na kufanya matendo yasiyokuwa na staha kama baba wa watoto wake.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments