Hamis wa BSS amuangukia Harmonize "Naomba Anisamehe Nilidhani Nimeshatoboa"
Ni 'headlines' za Hamis wa BSS msanii aliyejipatia umaarufu kupitia mashindano ya kusaka vipaji Bongo, ameonekana kumwaga machozi kwa boss wa lebo ya Konde Gang Harmonize huku akitaka msaada kutoka kwa msanii huyo.

Hamis Bss amefika mbali zaidi kwa kusema kama msanii huyo amemkosea basi anaomba amsamehe kwani mwanzo alionesha nia ya kutaka kumsapoti wakati alipokuwa kwenye mashindano.

"Ningeomba sana anisaidie, ujue mpaka mtu anafikia hatua ya kulia kwa ajili ya kuomba msaada sio poa, anisadie kwa chochote kile hata kwa wimbo mmoja au video tu kwa sababu anajuana na watu wengi, alivyosemaga kwamba atanisaini na kunisaidia nilidhani nimeshatoboa au kama nimemkosea naomba anisamehe" ameeleza Hamis

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments