Huu Hapa Ukweli Mchungu "Shule Haikuandai Kufanikiwa KIFEDHA Bali Inakuandaa Kuwa Tegemezi"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Tokea tukiwa wadogo tumeshuhudia wazazi na walezi wakituaambia tuende shule ili tupate kazi. Ni kweli walikuwa wanasema vitu vyenye uhalisia japo wenyewe walikuwa hawajui kama wanachosema ndio halisi.


Mafanikio ya kifedha yanataka maarifa ya kifedha yenye uhalisia, mtaalamu wa elimu ya fedha Steve jobs amewahi kusema, "Ili mtu ufanikiwe kifedha unatakiwa kila mwaka usome walau vitabu 12 vya elimu ya fedha." Sasa jiulize wewe unasoma vingapi kwa mwaka vitabu vyenye maarifa ya kifedha ili ufanikiwe kifedha.


Kufanikiwa kifedha ni kujua vyanzo halali vya fedha na namna ya kuiendesha fedha na kuidhibiti fedha ipasavyo. Ukiwa na fedha mkononi na ukajikuta unaitumia yote bila kuweka akiba na huna rekodi nzuri ya ulichotumia ni kipi, hiyo ni ishara kuwa wewe huwezi kufanikiwa kifedha. Watu wengi wanadhani mafanikio ya kifedha ni kupata fedha tu bila kujua namna ya kuiendesha.


Ili ufanikiwe kifedha kwanza uwe na uwezo mkubwa wa kupangilia mapato na matumizi bila kusahau akiba ya unachokipata. Mtu yoyote ambae matumizi yake yanazidi mapato yake huyo kamwe hawezi kufanikiwa kifedha. Mtu yoyote ambae haweki akiba huyo hawezi kufanikiwa kifedha. Ili ufanikiwe kifedha unatakiwa maeneo yote haya tuliosema kuyadhibiti ipasavyo.


Elimu hii shule haifundishwi kabisa ili upate elimu hii, unatakiwa kusoma vitabu vya ziada ambavyo wengi wetu hatuna tamaduni ya kusoma. Mafanikio ya kifedha sio uchawi wala sio ngekewa, mafanikio ni kuishi na kanuni na mikakati ya kifedha ndio ufanikiwe kifedha. Utaajiriwa mpaka kufa kama hautotambua vyema maarifa ya kifedha. Ajira sio mbaya ila inadumaza ubongo na kuishi ukiwa mtumwa.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad