1/24/2021

Mapya ya CUF kuhusu Kusambaratika Kisa Maalim Seif

 


Chama cha wananchi (CUF) kimekanusha taarifa zinazosambaa zikidai kuwa chama hicho kimesambaratika na kufa ilihali bado wanachama wa chama hicho wapo wakiendelea na majukumu ya kukijenga chama.

 

Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 24, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazee CUF, Mohamed Chunga, amesema madai kuwa Maalim Seif Hamad amesambaratisha chama hiko ni ya uongo kwani Maalim sio muasisi wa chama na hana uwezo  wa kusambaratisha huku akiwataka wanachama sambamba na watanzania kupuuza taarifa hizo. 


"Sisi Chama Cha Wananchi, CUF - Wazee, taarifa hizo ni za uzushi na hazina maana yeyote kwasababu chama ni watu na wanachama, na wanachama wa CUF wapo na hata uchaguzi ulipofanywa bado tuna wabunge wawili tumewapata sasa anaposema chama kimekufa tunashangaa" amesema Mzee Chunga


Aidha Mohamed Chunga amesema wataendelea kuhamasisha na kulinda amani na utulivu nchini pamoja na kuimaraisha chama chao huku wakizingatia misingi iliyowekwa katika kuendeleza na kudumisha demokrasia nchini.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger