Masau Bwire "Niombeeni nimekamatika haswa! Nimeambiwa nimekula chakula chenye sumu"

advertise here

OFISA Habari wa Ruvu Shooting inayoshiriki Ligi Kuu Bara amewaomba Watanzania wamuombee kwa kuwa kwa sasa hali yake haijatengamaa kwa kile ambacho ameambiwa na madaktari kuwa amekuwa chakula chenye sumu.

Kupitia ukurasa wake wa Istagram Masau Bwire ameandika: Kwa siku kadhaa zilizopita, nimekuwa sipokei simu, au nikipokea nasema tu siko vizuri, siwezi kuzungumza! Wapo walionielewa, lakini wapo walioona kama ni jeuri na kiburi tu, nafanya makusudi, kwa sababu sitaki kuzungumza nao.


Niwaombe radhi, wanisamehe kwa yote, lakini pia niwaaambie, na kuwahakikishia kwamba, sina kawaida hiyo ya kutopokea simu ya mtu yeyote atakayenipigia, siwezi kudharau simu ya mtu yeyote, daima namuomba Mungu, aniepushe na tabia hiyo ya kishetani ya kudharau na kutowapa ushirikiano pale wanapohitaji lolote kutoka kwangu.


Kwa kweli nilikuwa katika hali ngumu, kama unavyoiona hiyo picha, ndio uhalisia wa namna nilivyokuwa, nilikamatika haswa! Baada ya vipimo vya Hospitali, wataalamu wa afya (Daktari), walinambia, nilikula chakula ambacho hakikuwa salama,  chenye sumu!


Mwili pamoja na kwamba, haujawa na nguvu ya kutosha, hata kazini bado sijaweza kwenda, namshukuru Mungu, kwa kweli sijambo, naendelea vizuri.


Nikumbukeni katika maombi.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE