Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Mshahara wa Chikwende Kufuru Simba
UNAWEZA kusema ni kufuru mara baada ya uongozi wa Simba kukubali kumpa staa mpya wa timu hiyo, Perfect Chikwende mshahara wa dola za Kimarekani 8,000 ambazo ni sawa na Sh 18,470,900 za Kitanzania.

 

Chanzo cha kumaminika kutoka ndani ya Simba, kilieleza kuwa ulitokea mvutano mkubwa kwenye mshahara huo ambao Simba walitaka kumpa dola 6,000 (Sh 13,853,200), lakini jamaa akaweka ngumu akitaka dola 8,000 huku akiwaambia kama wakishindwa atakwenda zake Azam ambao walikuwa tayari kutoa mpunga huo.Kikizungumza na Spoti Xtra, chanzo hicho kilisema mshahara wa Chikwende ni mkubwa zaidi pengine kuliko wachezaji wengine.

 

“Chikwende atakuwa analipwa dola za Marekani 8,000, ambazo ni zaidi ya Sh milioni 18 za Kitanzania, Simba walikuwa wanataka wampe chini ya hapo, kwenye dola 6,000 au 5,000, lakini jamaa akagoma kabisa akidai kama wakishindwa kumpa anachotaka atakwenda zake Azam,” kilisema chanzo hicho.

 

Simba imesajili Chikwende kwa mkataba wa miaka miwili unaotajwa kufikia thamani ya dola 55,000 ambazo ni sawa na Sh 126,987,000 na inaelezwa kama Simba wangezubaa kidogo mwamba huyo alikuwa anatua ndani ya Azam FC.


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments