Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Penzi la Harmo na Kajala Mapya Yaibuka

LICHA ya muigizaji Kajala Masanja kunanusha vikali kuwa na uhusiano wa kimapenzi na staa wa Bongo Fleva, Rajabu Abdul ‘Harmonize’, penzi linalowahusisha wawili hao limeibua balaa kama lote kwenye mitandao ya kijamii hususan Instagram.

 

Kwenye mitandao ya kijamii, Harmo wamekuwa wakihusishwa kuwa ndio kapo mpya hivyo kuleta mijadala mbalimbali kwa wafuatiliaji wa mitandao.

 

“Kwa nini Harmo kila uchwao ni kumposti Kajala? Hapa si bure,” baadhi ya maoni yanayotembea kwa kasi mitandaoni.Balaa jipya ameliibua juzikati Harmonize au Harmo baada ya kuposti kwenye Instagram kupitia kipengele cha Insta-Story kwa kuandika ‘I Love You Kajala’ na kusindikiza na alama za makopa pamoja na alama na kuashiria kulia.

 

Baada ya posti hiyo, watu wengi walisema huenda zile tetesi za kwamba wawili hao ni wapenzi kwa kuwa mara kadhaa Harmo amekuwa akimposti Kajala kwa lugha za kuonesha upendo.Hata hivyo, Kajala kwenye moja ya mahojiano aliyoyafanya mwishoni mwa mwaka jana na magazeti Pendwa, alikataa katakata kuwa hana uhusiano na Harmo.

 

Akizidi kujitetea Kajala alisema, kama angekuwa na uhusiano na Harmo basi asingempeleka polisi wakati fulani alipomkosea.Ushadadiaji wa jambo hilo umekuwa mkubwa hasa kufuatia uwepo wa taarifa za kwamba Kajala amegombana na mtu wake ambaye ndiye alikuwa akimpa jeuri mjini.Mtu huyo anatajwa kwa sasa kuwa na mahusiano na mtu mwingine hivyo kuwepo na uwezekano mkubwa wa Kajala kujituliza na Harmo. Ni suala la muda, tusikilizie tutaupata ukweli!

 

TUJIKUMBUSHE

Harmo alianza kuibua mjadala juu ya watoto wa wazuri kutoka Bongo Muvi akiwemo Kajala kabla ya Sikukuu ya Krismasi, Disemba 25 mwaka 2020.

 

Kupitia kipengele cha Insta Story, Harmo aliwaposti warembo wakiongozwa na Wema Sepetu, Kajala, Irene Uwoya, Aunt Ezekiel, Hamisa Mobeto, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Jacqueline Wolper na Mimi Mars.

 

Gumzo likaanza hapo ambapo watu walijiongeza kwa kusema, kwa nini awaposti warembo hao na zaidi ilikuwa ni kwa Kajala ambaye tetesi zilikuwa zimezagaa kuwa ni mtuwe.

 

Pamoja na Kajala kukanusha, kwenye mkesha wa Mwaka Mpya, Harmo alionesha kwamba bado ‘hakomi’ kwani alimposti tena Kajala kwenye Insta-Story na kusindikiza na maneno yalisosomeka: “My family.”

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments