Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Polisi wasimulia Tembo alivyoteketeza familia ya 3

 


Watu watatu wa familia moja, mume, mke na mtoto wao, wamepoteza maisha na mwingine mmoja kujeruhiwa, Januari 3, 2021, majira ya saa 11:00 jioni, baada ya kuvamiwa na kushambuliwa na Tembo katika Kijiji cha Nshabaiguru, Kata ya Kihanga wilayani Karagwe, mkoa wa Kagera.


Kamanda wa polisi mkoani Kagera, Revocatus Malimi, amesemema kuwa tukio hilo lilitokea Januari 03, 2021, majira ya 11:45 jioni na kutaja waliopoteza maisha kuwa ni Fred Muhire (45), baba wa familia aliyekuwa akifanya kazi ya kuchunga Ng'ombe, mke wake aitwaye Aneth Fred (33) na mtoto wao Angel Fred mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi sita.


"Mume wa mama huyo wakati akiendelea na shughuli zake alipata taarifa ya familia yake kuvamiwa na Tembo na kukimbia kwenda kutoa msaada, lakini naye alivamiwa na kushambuliwa na Tembo hao akapoteza maisha papo hapo na mwili wake ulipatikana Desemba 04, 2021" amesema Kamanda Malimi.


Aidha amemtaja majeruhi kuwa ni Juma Rashida (18) anayefanya kazi ya kuchunga Ng'ombe, ambaye amelazwa katika hospitali ya Nyakahanga akiendelea na matibabu.


Amesema siku ya tukio mama huyo aliondoka kwenda kisimani kuchota maji akiwa amembeba mwanae mgongoni na ghafla walikutana na kijana mmoja wa kijijini hapo akifukuzwa na Tembo, ambaye alimfikia mama huyo na kuwaheruhi vibaya.


Kamanda huyo amesema kuwa majeruhi hao walikimbizwa na kulazwa katika hospitali ya Nyakahanga na kuwa walipoteza maisha usiku.


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments