Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Prof. Jay: Siyo Lazima Uimbe Matusi
MSANII mkongwe wa Hip Hop Bongo, Joseph Haule maarufu kama Prof. Jay, amewakemea wasanii kuendekeza kuimba mambo ya chumbani katika nyimbo zao.

 

 

 

Ameeleza hayo kupitia ujumbe ambao ameuchapisha kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii ambapo amesema ili msanii afanikiwe kimuziki siyo lazima aimbe mambo hayo.

 

 

 

“Siyo lazima kila siku uimbe matusi na mambo ya kitandani ili wimbo wako uwe mkubwa na upendwe, bali unaweza kuimba wimbo wenye mafunzo mema kwa jamii na wadau wakakushika mkono kwa kiwango cha juu kabisa, Kwa pamoja tunaweza tukakiokoa kizazi hiki,” ameandika Prof. Jay.Ikumbukwe kwa sasa Prof. Jay anafanya vizuri na wimbo unaokwenda kwa jina la ‘Baba’ ambao ameshirikishwa na Stamina. Video ya wimbo huo inafanya vizuri  kwa hivi sasa kupitia mtandao wa YouTube  na ndiyo video inayotazamwa zaidi tangu ilipotoka ikiwa inashika namba moja.


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments