Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Simu na kamera zapigwa marufuku katika vituo vya kupiga kura Uganda

Tume ya uchaguzi nchini Uganda imepiga marufuku wapiga kura kwenda na simu au kamera kwenye kituo cha kupiga kura wiki ijayo tarehe 14 au kubaki kituoni kusubiri matokeo, agizo hilo limetolewa jana na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Jaji Simon Byabakama mjini Kampala.

Huku mashirika yasiyo ya serikali yakitaka tume kufafanua kuhusu teknolojia itakayotumiwa katika uchaguzi mkuu zikiwa zimesalia siku saba kufanyika zoezi hilo.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini Uganda Jaji Simon Mugenyi Byabakama ametangaza kanuni zitakazotumiwa katika uchaguzi huo, ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku waandishi habari kuingia ndani kwenye vituo vya kupiga kura ,kuvaa sare za chama chochote cha siasa au za mgombea yoyote, simu za mkononi pamoja na kamera 

Agizo la Jaji Byabakama kuzuia wapiga kura kubaki kwenye vituo vyao vya kupiga kura zinakinzana na zile za baadhi ya wagombea wa kiti cha rais ambao wamesikika katika kampeni zao za uchaguzi wakiwataka wafuasi wao baada ya kupiga kura wabaki kituoni kulinda kura zao.

Mwenyekiti wa tume ameongeza kuwa wapiga kura wakibaki kwenye vituo vya kupiga kura watasababisha msongamano mkubwa wa watu na kuvunja kanuni za watalaam wa afya za kudhibiti virusi vya corona.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

2 Comments

 1. Piga kura yako, Nenda nyumbani kwako.
  Wewe mmpiga kura, Si mgombea wala si Mshindaji mbio.

  Nenda katafute Riziki yako na Wanao.

  Fata na Zingatia Masharti ya Kolona na Maambukizi.

  Tunakutakieni Amani na Utulivu ndugu zetu Waganda.

  ReplyDelete
  Replies
  1. Hivyo TCRA ya Uganda Inaitwa .? is it UCRA.??

   Inafaa kubadilishana Uzoefu katika Vipindi kama hivi vya Uchaguzi. Uvunjifu wa Amani na Uhamasishaji kama
   aliofanyaa Tilampu Fezi buku na wananchi wa nchi twita na Wazee wa SistaGlamu ni lazima UWAMINYIE .

   Bongo ilikuwa poa tu..Hamna Tairi wala Basi wala kituo cha mafuta kwa kukosa Amri ya Bonijako na Godilesi IKALA KWAOOOOO.. TCRA HONGERENI SANA KUTUVUSHA NA FITINA YA UCHAGUZI..Wasaidieni utaalamu ndugu zetu na partner zetu katika uchumi na Jumuia.

   Amani yao ndio Amani yetu.

   Delete
Emoji
(y)
:)
:(
hihi
:-)
:D
=D
:-d
;(
;-(
@-)
:P
:o
:>)
(o)
:p
(p)
:-s
(m)
8-)
:-t
:-b
b-(
:-#
=p~
x-)
(k)