Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Yanga Yatamba Ubingwa Ligi Kuu, Simba Kimataifa

 


DIRISHA la usajili lilifungwa rasmi Ijumaa usiku na kushuhudia timu za Simba na Yanga zikishusha wachezaji wapya na kuwatambulisha ikiwa umebaki muda mchache kabla ya dirisha hilo kufungwa.


Yanga ilifunga usajili wao kwa kuutambulisha usajili wa mshambuliaji wao mpya mwenye uraia wa Burundi, Fiston Abdoul Razak huku Simba wao wakimaliza na kiungo mshambuliaji raia wa Zimbwambwe Tatenda Perfect Chikwende.


Kutokana na sajili hizo viongozi wa pande zote mbili wameibuka huku kila upande ukijinasibu kuwa kwenye mawindo yake Simba ikijinasibu kwenda kimataifa huku Yanga wao wakitamba kusepa na kombe la Ligi Kuu.


Mjumbe wa kamati ya usajili wa Yanga Injinia Hersi Said yeye amesema: “Tumekamilisha usajili wa maboresho ndani ya dirisha dogo la usajili kwa lengo la kuushinda kombe la Ligi Kuu msimu huu,”


Kwa upande wa Simba Ofisa mtendaji mkuu (CEO) wa timu hiyo Barbara Gonzalez yeye amesema kuwa “Usajili wa Perfect Chikwende ni kwa ajili ya kuiongezea nguvu timu yetu katika safu ya ushambuliaji kuelekea katika michuano ya ligi ya Mabingwa Afrika ambayo tumetinga hatua ya Makundi,”


 

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments