Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Huu ndiyo ujumbe wa mwisho wa Nditiye kwa Ndugai

 


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, ameusoma hadharani ujumbe wa mwisho alioandikiwa na aliyekuwa mbunge wa Muhambwe Mhandisi Atashasta Nditiye, siku chache tu kabla ya mauti kumfika.

 

Hayo yamejiri hii leo Februari 13, 2021, jijini Dodoma alipokuwa akitoa hotuba wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa mbunge na aliyewahi kuwa Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano, aliyefariki dunia jana katika hospitali ya Benjamin Mkapa baada ya kupata ajali.


"Mwanzo mwa mwezi huu Nditiye aliniandikia meseji ikisema, Mh Spika heri ya mwaka mpya, namshukuru Mwenyezi Mungu kwa ajili ya uhai na nimekuwa na ibada maalum mbili za kukuombea kwa jinsi ulivyoniinua katika maisha yangu, Mungu aendelee kuwa upande wako", ameeleza Spika Ndugai.


Aidha ameendelea kusema, "Nadhani ulikuwa unaniaga rafiki yangu na mimi nikamjibu, asante sana hakika tumekuwa pamoja sana, Mungu wetu ni mwema hatatuacha kamwe, lakini leo tupo hapa tunamuaga mwenzetu kweli maisha haya kila mmoja wetu ajiandae kwa imani yake tuwe karibu na Bwana".

 DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE

Mwili wa Mhandisi Atashasta Nditiye, alizaliwa Oktoba 17, 1969, na mwili wake utasafirishwa kesho Februari 14, 2021, kupelekwa mkoani Kigoma kwa ajili ya mazishi.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments